




Tunapenda kuwakaribisha wote katika maonesho haya mpate huduma mbalimbali zinazotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Huduma za udahili kujiunga na masomo katika ngazi za Certificates, Diploma, Foundation Program, Bachelor Degrees, Master na PhD zinapatikana kwenye banda letu lililopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja, kuanzia saa tatu kamili Asubuhi mpaka saa Kumi na Moja jioni.