Call: +255 22 2668992

WAZIRI MKUU ATOA KONGOLE CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA

waziri-mkuu-atoa-kongole-chuo-kikuu-huria-cha-tanzania

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa, ametoa pongezi kwa Chuo kikuu Huria cha Tanzania kupitia kitengo cha Teknolojia Saidizi kwa wanafunzi wenye Mahitaji Maalum kwa kazi nzuri inayofanyika kuhudumia watu wenye mahitaji maalum.

Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo Julai 19, 2022, alipotembelea banda la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknojia yanayoratibiwa na kusimamiwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam ambapo katika banda hilo aliweza kukutana na mwanafunzi Bernadetha Msigwa mwenye ulemavu wa macho lakini ameweza kuandika kitabu.

Waziri Mkuu aliweza kushuhudia namna Bernadetha anavyoweza kutumia vifaa vya kiteknolojia kwa ufanisi mkubwa katika kufanya kazi zake, hivyo kutoa agizo la Msigwa kuchukuliwa taarifa zake kwa ajili ya kuangalia namna anaweza kupata nafasi ya utumishi ili aweze kutoa ujuzi wake kwa manufaa ya taifa hili.

Maonyesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknojia yanaratibiwa na kusimamiwa na Tume za Vyuo Vikuu nchini (TCU), yanafanyika kila mwaka, mwaka huu (2022) yanafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia Julai 18, 2022 na yanataajiwa kumalizika Julai 23, 2022 jijini Dar Es Salaam, ambapo taasisi zinazotoa huduma ya Elimu ya Juu, hushiriki katika kuonyesha huduma zao kwa jamii.