Call: +255 22 2668992

Uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), ukiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Elifas Bisanda

uongozi-wa-chuo-kikuu-huria-cha-tanzania-out-ukiongozwa-na-makamu-mkuu-wa-chuo-hicho-prof-elifas-bisanda
Uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), ukiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Elifas Bisanda, umekutana na kufanya kikao na uongozi wa benki ya NMB Plc, ukiongozwa na Meneja Mahusiano wa benki hiyo Ms. Rachel Kissui. Kikao hicho kimekutanisha jopo la wataalam wa pande hizo mbili na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo maswala yatayoimarisha zaidi mahusiano ya taasisi hizo kwa maslahi ya wateja na wadau wa taasisi hizo, kikao hicho kimefanyika Agosti 25, 2021 makao makuu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Kinondoni jijini Dar Es Salaam.