Call: +255 22 2668992

MADAWATI YA JINSIA, YAMULIKE UKATILI KUPITIA MITANDAO YA JAMII – DKT. NYON

madawati-ya-jinsia-yamulike-ukatili-kupitia-mitandao-ya-jamii-dkt-nyon

Makamu Mkuu wa chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Elifas Bisanda, amesema kuwa ukatili wa kijinsia si swala la wanawake pekee kama ambavyo imezoeleka, wanaume pia hufanyiwa ukatili hivyo madawati ya jinsia yasimulike zaidi upande mmoja na kusahau mwingine.

“Ukatili hutokea kwa jinsia zote, uongozi wa chuo hiki unapinga vikali ukatili wowote unaohusu maswala ya kijinsia ndiyo maana tumeamua kuanzisha dawati hili ili kuhakikisha jamii yetu inashughulikia ukatili wa aina yoyote unaohusu jinsia.” Amesema Prof. Bisanda.

Mitandao ya kijamii, yaorodheshwa kama sehemu mojawapo yenye matukio ya ukatili wa kijinsia kutokana na uwepo wa vitendo vinavyoumiza hisia za watu hasa wanawake.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni, wakati wa uzinduzi wa dawati la jinsia la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), akimuwakisha Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, Julai 31, 2023 makao Makuu ya chuo hiki, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

“Dawati la jinsia linatakiwa kuzingatia ukatili unaofanyika katika mitandao ya kijamii, ni aina ya ukatili ambao unazidi kuenea sasa nchini ambapo mtu anaweza kukutumia picha ambazo hupendi kuziangalia. Pia, kuweka picha ya mtu katika mitandao ya kijamii bila idhini ya muhusika na bahati mbaya zikaleta mijadala tofauti inayoweza kumuumiza muhusika, huo nao ni ukatili unaopaswa kuangaliwa.” Amesema Dkt. Nyoni.

Ameendelea kusema kuwa uanzishwaji wa madawati ya kijinsia katika vyuo vikuu na vya kati ni agizo kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa taasisi hizo ambazo zimekuwa ni vyanzo vya kuwajengea uwezo vijana katika utoaji wa huduma za kimaendeleo kwa usawa wa kijinsia.

Dkt. Nyoni, ametoa pongezi kwa Chuo hiki kwa kutekeleza kwa vitendo agizo la wizara kwa kuanzisha dawati hilo, uteuzi wa Mratibu na wajumbe lakini pia uwepo wa waratibu wa mikoa katika vituo vya mikoa vya chuo hiki nchini. Aidha ametoa pendekezo kwa madawati ya jinsia kupelekwa katika shule za msingi ili kusaidia watoto wanaokosa elimu ya kijinsia na kupelekea kukumbana na ukatili wa kijinsia katika jamii zao.

Makamu Mkuu wa chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Elifas Bisanda, amesema kuwa ukatili wa kijinsia si swala la wanawake pekee kama ambavyo imezoeleka, wanaume pia hufanyiwa ukatili hivyo madawati ya jinsia yasimulike zaidi upande mmoja na kusahau mwingine.

“Ukatili hutokea kwa jinsia zote, uongozi wa chuo hiki unapinga vikali ukatili wowote unaohusu maswala ya kijinsia ndiyo maana tumeamua kuanzisha dawati hili ili kuhakikisha jamii yetu inashughulikia ukatili wa aina yoyote unaohusu jinsia.” Amesema Prof. Bisanda.

Mratibu wa dawati hilo la jinsia la OUT, Dkt. Lilian Macha, amesema utekelezaji wa majukumu ya dawati hili ni nyeti na yanahitaji uangalivu mkubwa, ameahidi kuwa watatekeleza shughuli za dawati hilo kwa kuzingatia nidhamu, haki na usawa ili kuepusha migogoro katika jamii hii.

Hafla ya uzinduzi wa Dawati hilo imekwenda sambamba na mgeni rasmi, Dkt. Nyoni kukabidhi madaftari maalum kwa ajili ya kurekodi kumbukumbu za matukio ya ukatili endapo yatatokea chuoni.